Wapenda SOKA (Kandanda)

Swahili is the main language of Wapenda SOKA (Kandanda) facebook group. Having alot of group type in Facebook: close, open and secret and it is a CLOSED group. They attracted 15,198 members. So it is a Huge group. 107934682613092 is the identifier of this group with Facebook. We last updated on 2015-01-30 09:04:13.

KUHUSU KUNDI:
[1] WAPENDA SOKA ni kundi linalounganisha jumuiya kubwa ya mashabiki na wapenzi wa soka wa rika,vyeo,rangi,jinsia,na itikadi mbalimbali,lengo ni kukutana pamoja na kujadili soka

[2] Kila mwanachama ana haki ya ku-Add au kumuongeza mtu yeyote ndani ya kundi hili,lakini kila mwanachama mpya atakayoongezwa hupata haki"Administrative Approval" toka kwa kiongozi yeyote wa kundi hili.

[3] Matumizi ya matusi ya aina zote,lugha chafu,kashfa hasi,lugha za kichochezi ni marufuku katika kundi hili

[4] Kauli zozote za ubaguzi wa kijinsia 'sexual abuse',kidini,kirangi 'racial abuse',kikabila,kitabaka na zingine zenye kufanana na hizo haziruhusiwi

[5] Post au comment za aina yeyote ile ya mlengo wa biashara au promo ya kitu chochote ni lazima zipate kibali toka kwa Admins ,kinyume na hapo si ruhusa kuweka tangazo la biashara,kutangaza blog,kutangaza kundi lingine la soka,kuweka link za blog za watu binafsi(ni sharti link ya blog au website yeyote iambatane na habari kamili iliyoandikwa na muweka post,na link iwe kama msomaji ataamua kufungua) kinyume na hapo post itataolewa

[6] Kebehi hasi,ndelemo,vifijo,utani hasi,vijembe hasi na chachandu zote za mchezo wa soka ni ruksa ndani ya kundi hili,bila kuvunja sheria na kanuni.

[7] Kundi hili na utawala wake hautahusika na uvunjaji wa sheria halali za JAMUHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA utakaofanyika ndani ya kundi hili na litakuwa tayari kutoa ushirikiano kulinda na kusimamia sheria halali za nchi.

MWONGOZO WA ADMINS:

[1] Kundi hili lina Admins watano(5),kwa majina Richard Mkambala,Edo Daniel Chibo,Bebeng Stearling,Allen Kaijage,Patrick Absalom,Abel Chimwejo na Dan Chibo(Mwenyekiti wa Admin Pannel na Founder wa kundi)

[2] Kila Admin anapaswa kutenganisha kofia ya ushabiki wa klabu au timu anayoipenda na utawala kwa kufanya kazi bila kuweka hisia na mapenzi ya klabu yeyote ndani yake,lakini si kuacha kushabikia timu yake hiyo ni haki yake ya msingi.

[3] Admin yeyote haruhusiwi kutoa post au comment ya mtu yeyote yule ambaye hajavunja kanuni au sheria yeyote ya kundi hili.

[4] Admin anaruhusiwa kumtoa mwanachama yeyote kwenye kundi ambaye haendani na sheria za kundi au uwepo wake unavunja amani ya kundi na kisha kuwajulisha Admins wenzake na ikiwezekana kutoa tangazo kwa members wote kama itahitajika..

NB: Inampasa kila mwanachama kuzisoma na kuzijua sheria na taratibu zote za kundi,hakutakuwa na sikujua,"ignorance of law is not an excuse".